25 Februari 2017 - 19:14
Waziri wa mambo ya nje ya Saudia azuru Iraq

Licha ya serikali ya Saudia arabia kuonyesha bayana kuwa inaunga mkono magaidi wa Daesh ambao wanafanya jinao nchini Iraq na Syria, Waziri wa masuala ya kigeni wa Saudi Arabia, Adel Al-Jubeir leo hii amefanya ziara ya nadra nchini Iraq

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Licha ya serikali ya Saudia arabia kuonyesha bayana kuwa inaunga mkono magaidi wa Daesh ambao wanafanya jinao nchini Iraq na Syria, Waziri wa masuala ya kigeni wa Saudi Arabia, Adel Al-Jubeir leo hii amefanya ziara ya nadra nchini Iraq na kukutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Haider al-Abadi, taarifa ya ofisi ya waziri mkuu imesema. Msemaji wa wizara ya masuala ya kigeni wa Iraq, ameongea na waandishi wa habari  kwamba hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi mwandamizi kutoka Saudi Arabia tangu kufanyika kwa uvamizi wa kijeshi ulioongozwa na Marekani uliomuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Saddam Hussein mwaka 2003. Saudi Arabia ilifungua tena ubalozi mjini Baghdad mwaka mmoja uliopita baada ya kufungwa kwa miaka 25. Lakini Iraq ilitaka kubadilishwa kwa balozi baada ya aliyekuwepo kutoa matamshi ya kuunga mkono magaidi wa Daesh wanaoua wananchi wa Iraq na Syria nakudai kuwa Iraq inatesa waislamu wa dhehebu la Sunni, matamshi ambayo yaliwaghadhabisha wanasiasa na viongozi na waislamu dhehebu ya Shia ambao ni wengi nchini Iraq. Taarifa zilizotolewa leo hii na wizara ya masuala ya kigeni ya Iraq imesema Saudi Arabia imekubali kuteua balozi mpya wa nchi hiyo. Hatua hii imekuja wakati majeshi ya Iraq yakisaidiwa na wataalamu wa masuala ya kijeshi kutoka Iran wakiendelea kupata ushindi mkubwa dhidi ya magaidi wa Daesh katika mji wa Mosul.

Mwisho wa habari/ 291