Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa masuala ya kigeni wa Mexico Luis Videgaray amesema Mexico inaweza kuzitoza kodi bidhaa za Marekani kwa kulipiza kisasi, ikiwa jirani yake huyo wa upande wa Magharibi ataziwekea ushuru bidhaa zinazoingizwa Marekani kutoka nchini mwake ikiwa ni hatua ya kuigharamia ahadi ya Rais Donald Trump ya ujenzi wa ukuta mkubwa wa mpaka kati ya nchi hizo. Videgaray amenukuliwa hapo jana kwenye mahojiano na kituo cha redio akisema kwamba hawawezi kufunga mikono na kutochukuwa hatua. Waziri wa mambo ya ndani Miguel Angel Osorio Chong amesema, Mexico inaweza kuhimili hatua zozote za kuondolewa kwa ufadhili wa masuala ya usalama kutoka kwa Marekani, na maafisa wameiita fikra ya kipuuzi ya Marekani kwamba inaweza kuwarejesha nchini humo wahamiaji wasio wa Kimexico. Mwezi Januari rais wa nchi hiyo Enrique Pena Nieto aliahirisha ziara yake nchini Marekani, wakati Trump akiendelea kusisitiza kwamba Mexico italipia gharama za ujenzi wa ukuta huo.
Mwisho wa habari/ 291