Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Yusuf Rabie ambaye ni mkuu wa kitengo cha kutetea haki za binadamu nchini Bahrain amekemea vikali kitendo cha maafisa wa usalama wa Bahrain kuivamia nyumba ya mwanaharakati anayetetea demokrasia na haki za wananchi wa Bahrain sheik Issa Qassim, na kuizingira nyumba hiyo.
Maafisa wa usalama wa Bahrain wamewashambulia vikali wananchi waliokuwa wanajaribu kusogea karibu na nyumba ya mwanaharakati huyo ambaye anapinga dhuluma zinazofanywa na serikali dhidi ya wananchi wasiojiweza wa Bahrain ambao wamekuwa wakiandamana kutaka haki zao tangu mwaka 2011, ambapo majeshi ya Saudia Arabia yakisaidiwa na majeshi ya Uingereza yamekuwa yakiwazuia wananchi hao na kuwafunga na wengine kuvuliwa uraia wa nchi hiyo na kuwahamishia nchi nyingine ili wasiweze kuendeleza harakati zao za kudai demokrasia.
Wafuasi wa sheik Issa Qassim wameonya kuwa endapo sheikh huyo atadhulika basi watachukua hatua kali dhidi ya serikali ya nchi hiyo ya kifalme.
Mwisho wa habari / 291