28 Mei 2017 - 20:48
 Watu tisa wauawa katika mlipuko wa bomu Baghdad

Watu tisa wameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga huku wengine 12 wakijeruhiwa vibaya leo hii katika mji wa Baquba,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Watu tisa wameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga huku wengine 12 wakijeruhiwa vibaya leo hii katika mji wa Baquba, ulioko Kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq Baghdad. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa duru za kipolisi na watoa huduma za afya. Mtu mmoja aliyejivisha mkanda wenye mabomu alijilipua katikati ya mtaa uliofurika watu mjini Baquba katika mkoa wa Diyala duru nyingine zimeliambia shirika la habari la dpa kwa masharti ya kutotajwa jina. Polisi imesema idadi ya vifo imefikia 10 ikiwa ni pamoja na mshambuliaji. Hadi sasa hakuna taarifa za kuhusika kwa kikundi lolote. Diyala iliyoko kiasi cha kilomita 57 Kaskazini mwa Baghdad, imeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara katika siku za hivi karibuni yanayofanywa na kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu IS ambalo linadhaminiwa na Saudia arabia na washirika, ambalo lilifurushwa na vikosi vya serikali kutoka eneo hilo takriban mwaka mmoja uliopita.

Mwisho wa habari/ 291