Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Muungano wa nchi za kiarabu umeamua kuitenga serikali ya Qatar kutokana na nchi hiyo kuunga mkono serikali ya Iran na mapambano ya Iran dhidi ya magaidi.
Shirika la habari la Kuwait KUNA limeripoti kwamba Mfalme wa nchi hiyo yuko njiani kuelekea Saudi Arabia kwa kile ambacho maafisa wa Ghuba wamekitaja hapo mapema kwamba ni ziara ya mazungumzo na mfalme Salman wa Saudi Arabia kuhusiana na mgogoro wa nchi za kanda hiyo ya Ghuba ya kiarabu na Qatar.Sheikh Saba anatarajiwa kuwasili Jeddah kama msuluhishi kati ya Qatar na nchi kadhaa zilizoingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na uhusiano wa shughuli za kiusafiri,ikiwemo Saudi Arabia. Taarifa zimeeleza kwamba leo Saudi Arabia na Bahraine zimefutilia mbali leseni ya shirika la ndege la Qatar na kulitka shirika hilo kufunga ofisi zake zote katika kipindi cha saa 48.Kadhalika shirika la habari la Bahrain BNA limetangaza taarifa inayowataka abiria wote waliokata tiketi za kuelekea au kutoka Qatar kuwasiliana na ofisi za shirika hilo la ndege kurudishiwa fedha zao katika kipindi cha saa 48.Saudi Arabia,Umoja wa Falme za kiarabu,Misri,Bahrain na Yemen zote zimetangaza kuuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Qatar.Sambamba na hayo nchi hizo za Ghuba pia zimewataka raia wote wa Qatar kuondoka kwenye nchi hizo katika kipindi cha siku 14 huku Saudi Arabia ikiufunga mpaka wake na Qatar ambayo ni njia pekee ya usafiri wa barabara ya Qatar kuingiza chakula.
Adhabu hii kali kwa Qatar inakuja katika kipingi ambacho rais wa Trump wa Marekani amemaliza ziara yake Saudia arabia ambapo aliwashawishi waarabu kuendelea kuitenga Iran. Serikali ya Qatar imepinga hoja kuwa Iran ni hatari kwa nchi za kiarabu na kuwashauri waarabu wachunguze vizuri adui yao ni nani.
Mwisho wa habari/ 291