6 Juni 2017 - 21:42
Serikali ya Uingereza iko tayari kuikabili nchi yoyote itakayothibitika kufadhili magaidi

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema nchi yake inahitaji kuwa na mazungumzo magumu na wale wote wanaofadhili ugaidi pamoja na itikadi kali ikiwemo serikali za kigeni sambamba na washirika wake ikihitajika.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema nchi yake inahitaji kuwa na mazungumzo magumu na wale wote wanaofadhili ugaidi pamoja na itikadi kali ikiwemo serikali za kigeni sambamba na washirika wake ikihitajika.Ametowa msimamo huo baada ya kuulizwa na kituo cha Televisheni cha Sky News iwapo atakuwa tayari kuzikabili serikali za kigeni au washirika wa Uingereza endapo itabainika zinahusika katika kuunga mkono makundi ya wanamgambo,baada ya nchi yake kushambuliwa na magaidi kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi kifupi.Mapema leo waziri wa mambo ya nje Boris Johnson alitangulia kusema kwamba Uingereza inahitaji kushirikiana na nchi nyingine kuzuia ufadhili wa ugaidi iwe ufadhili huo unatolewa na serikali hizo kwa kufahamu au kwa kutofahamu.

Ni kwa muda mrefu sasa, serikali ya Uingereza  imekuwa ikishirikiana na nchi za kiarabu katika kudhamini upande wa magaidi nchini Syria ili kuiangusha serikali ya rais Bashar asad.       

Mwisho wa habari / 291

 

Tags