24 Oktoba 2017 - 08:16
Majeshi ya Syria yakomboa mji wa Khuisham

Majeshi ya serikali ya Syria yamefanikiwa kukomoa mji wa Khusham kutoka mikononi mwa kikundi cha magaidi wa Daesh nchoni humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya serikali ya Syria katika muendelezo wa mashambulizi yake dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo, wamefanikiwa kukomboa mji wa Khusham uliopo mwanzoni mwa fukwe wa mto Furati.
Aidha majeshi ya Syria yamefanya mashambulizi katika ufukwe wa mashariki ya mto Furati na kushambulia maeneo yalikuwa yanakaliwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Khusham na baada ya masaa kadhaa ya mashambulio hayo, waliweza kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa kikundi hicho cha kigaidi.
Hivi majeshi ya Syria baada ya kuukomboa mji wa Khusham, wanasonga mbele wakiendeleza mashambulizi yao dhidi ya magaidi Daesh katika sehemu zilizobaki zinazokaliwa na magaidi hao katika fukwe za mashariki ya mto wa Furati.
Kwa upande mwingine majeshi ya Syria inaendelea kufanya mashambulizi pembezoni mwa mji wa Almayadin dhidi ya magaidi wa Daesh ambapo katika upande wa kusini mwa mji huo wamefanikiwa kuukomboa mji wa Quriyah kutoka mikononi mwa kikundi cha Daesh nchini humo.
mwisho/290