Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Israel leo usiku vimetangaza kushambuliwa kwa eneo la kusini mwa Israel kwa kombora liliotoka ukanda wa Gaza nchini Palestuna.
Majeshi ya utawala haramu wa Israel katika masiku ya hivi karibuni vimefanya mashambulizi ya makombora katika maeneo ya ukanda wa Gaza nchini Palestina.
Katika mashambulio ya hivi mwishoni ambapo makumi ya wananchi wa Palestina wamepoteza maisha na kujeruhiwa.
Hayo yametokea baada ya Trump “Rais wa Marekani” kutangaza kuwa Quds ndio mji mkuu wa Israel na ubalozi wake atauamisha kutoka Telaviv na kuupeleka Quds ya Palestina, jambo ambalo limesababisha kukua kwa mashambulio baina ya Israel na vikundi vya mapambano vya Palestina.
Maamuzi ya Trump yamepingwa na mataifa mbalimbali ulimwenguni, ambapo kwa upande mwingine jamii za Kiislamu na wapenda haki kila pande ulimwenguni wamepaza sauti ya kupinga maamuzi ya Rais wa Marekani, walidhihirisha mitazamo yao kwa kufanya maandamano na wengine kujumuika katika sehemu mbalimbali.
mwisho/290
9 Desemba 2017 - 19:41
Msimbo wa Habari: 871792
Kombora mmoja kutoka ukanda wa Gaza lashambulia maeneo yaliojengwa na utawala wa kivamizi wa Israel kusini mwa Israel