Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jeshi la Syria limesema limeweka vikosi vyake katika mji wa Manbij kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, baada ya wanamgambo wa Kikurdi wa kundi la YPG kuitaka serikali ya kuulinda mji huo baada ya Marekani kuwatekeleza wanamgambo hao na kuvunja ahadi zote ilizowapa.
Hatua hiyo imekuja kutokana na kitisho cha mashambulizi kutoka majeshi ya Uturuki huku nchi hiyo ikipinga hatua hiyo iliyochukuliwa na wanamgambo hao. Uturuki imesema leo kwamba wanamgambo wa Kikurdi nchini Syria hawana haki ya kuomba msaada kutoka serikali ya Syria kupambana na kitisho hicho cha mashambulizi kutoka Uturuki upande wa kaskazini.
Wanamgambo wa kundi lijiitallo Vikosi vya Ulinzi wa Umma, YPG, vinavyodhibiti eneo hilo kwa silaha hawana haki ama nguvu za kutoa taarifa ya kukaribisha makundi mengine kwa niaba ya watu wa eneo hilo, imesema wizara ya ulinzi ya Uturuki.
Vikosi vya serikali ya Syria vilivyopelekwa katika eneo la Manbij vimeingia katika mji wa Manbij kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Syria brigedia jenerali Ali Mayhoub.
"Taarifa ya mamlaka kuu ya jeshi la Syria, kwa misingi ya jeshi la ulinzi na dhamira yake ya jumla kuhusiana na jukumu la utekelezaji wa ulinzi wa kila sehemu ya mipaka ya jamhuri ya Syria, na kujibu miito ya watu wa Manbij, majeshi ya ulinzi yametangaza kwamba wapiganaji wa jeshi ya Syria wameingia Manbij na kupandisha bendera ya jamhuri ya Kiarabu ya Syria."
Marekani imewasaliti wakurd
Uamuzi wa ghafla wa rais wa Marekani Donald Trump kuviondoa vikosi vya jeshi la nchi hiyo kutoka Syria kumewatia shaka wapiganaji wanaoongozwa na Wakurdi ambapo Marekani iliwatumia kama ngao ya kujipatia manufaa yake nachini Syria.
Mwisho wa habari / 291