Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyanzo makini vya habari nchini humo Ijumaa ya leo imetangaza kufa kwa wanajeshi 10 wa Emirates baada ya kutokea mashambulizi makali baina yao na makabila yaliopo katika mkoa wa Al-shabuh kusini mwa mashariki ya Yemen.
Alkadhalika Televishen ya Aljazira ya Qatar bila ya kubainisha zaidi, imetangaza kuwa, miongoni mwa wanajeshi waliokufa ni makamanda kadhaa wa majeshi ya Emirates.
Kwa upande mwingine ripoti kutoka kwa vyombo vya habari vya sehemu iliotokea tukio hilo vinaashiria kuwa katika mashambulio hayo ndege za Emirates pia zilishiriki.
Inasemekana kwamba katika miaka ya hivi karibuni makumi ya wanajeshi wa Emirates wamepoteza maisha katika maeneo mbali nchini Yemen.
mwisho/290
4 Januari 2019 - 17:32
Msimbo wa Habari: 923536
Kufuatia mapambano yaliotokea nchini Yemen kati ya majeshi ya Emirates na makabila yaliopo katika mkoa wa Al-Shabuh kusini mwa mashariki ya Yemen na kusababisha kuangamia kwa wanajeshi 10 wa mamluki wa Emirates