Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri mkuu wa China Li Keqiang ametoa angalizo kwamba nchi hiyo itakabiliana na hali ngumu kiuchumi, wakati akiwasilisha hatua za kupunguza kodi kujaribu kuuchochea uchumi unaolegalega na huku pia akiongeza matumizi ya jeshi kwa takribani dola bilioni 180. Kupungua kasi ya ukuaji wa uchumi pamoja na vita vya kibiashara na Marekani kumekuwa ni changamoto kubwa kwa Rais Xi Jinping, mwaka mmoja baada ya kuwa kiongozi huyo mwenye nguvu nchini humo tangu enzi za utawala wa Mao Zedong kwa kuondoa ukomo wa muhula wa kuwapo madarakani na kuweka jina lake katika katiba ya nchi hiyo. Waziri Mkuu Li Keqiang amekiambia kikao cha ufunguzi cha mkutano mkuu wa taifa nchini China kwamba serikali inalenga kupata ukuaji wa uchumi unaofikia asilimia 6.0 hadi 6.5 mwaka huu, ikipunguza kiwango chake kutoka mwaka 2018. Karibu wajumbe 3,000 nchini humo wanahudhuria mkutano huo wa wiki mbili, wenye lengo la kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wa nje.
Kwasasa China ni nchi yenye uchumi wajuu hasa kwa kuzingatia sekta ya viwanda, na imejikuta kwenye vita na mataifa makubwa ambayo hayataki nchi nyingine zikue kiuchumi.
Mwisho wa habri / 291