15 Juni 2019 - 07:42
Kituo cha kidini cha Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia mjini Vienna kupigwa kufuli rasmi

Bange la Austria limepitisha kwa wingi wa kura mpango wa kukipiga kufuli kituo cha kidini cha Mfalme Abdullah wa Saudia mjini Vienna.

(ABNA24.com) Bange la Austria limepitisha kwa wingi wa kura mpango wa kukipiga kufuli kituo cha kidini cha Mfalme Abdullah wa Saudia mjini Vienna.

Bunge hilo lilichukua uamuzi huo Jumatano ya jana katika kikao cha awali cha pamoja kati ya serikali mpya na wabunge, ambapo liliupitisha kwa wingi wa kura mpango wa chama cha 'Sasa' wa kukifunga kituo hicho kilichozusha utata kilichofunguliwa mwaka 2011 na Saudia mjini Vienna kupitia fedha za ukoo wa Aal Saud. Kituo hicho chenye utata kilifunguliwa na Saudia kwa lengo la kile kilichotajwa kuwa ni kwa ajili ya mazungumzo ya kidini nchini Austria jambo ambalo liliendelea kupingwa na jamii ya nchi hiyo.

Katika uwanja huo Alexander Schallenberg, Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria amesema kuwa, hatua zote za kisheria za kupigwa kufuli kituo hicho cha Mfalme Abdullah wa Saudia zimechukuliwa. Aidha wawakilishi wa vyama vya Social Democratic, Uhuru na 'Sasa' wameupasisha kwa wingi wa kura mpango wa kufungwa kituo hicho cha Saudia. Peter Pilz, mkuu wa chama cha 'Sasa' ambaye ndiye aliwasilisha bungeni muswada wa kufungwa kituo hicho cha Saudia mjini Vienna amesema kuwa, ni lazima kituo hicho kiwe kimepigwa kufuli kamili ndani ya siku 14 zijazo. Akiashiria suala hilo Peter Pilz amesema kuwa hatua ya pili kwa serikali ya Vienna itakuwa ni kuupiga kufuli pia ubalozi wa Saudia nchini humo.



/129