(ABNA24.com) Subrahmanyam Jaishankar ameyasema hayo katika bunge la India na kuongeza kuwa, Pakistan imefumbia macho haki ya nchi yake ya kuuruhusu ubalozi mdogo wa India kuwasiliana na raia wake huyo aliyehukumiwa adhabu ya kifo nchini humo.
Hii ni katika hali ambayo mapema jana Imran Khan, Waziri Mkuu wa Pakistan alisema kuwa Jadhav ametenda jinai dhidi ya Pakistan na kusisitiza kuwa, raia huyo wa India atahukumiwa kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.
Wakati huo huo jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) ya The Hague sambamba na kutupilia mbali takwa la India la kutaka kubatilishwa hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama ya kijeshi ya Pakistan dhidi ya raia wake, aliitaka pia serikali ya Islamabad kuuwekea mazingira mazuri ubalozi mdogo wa India nchini humo uweze kuwasiliana na Kulbhushan Jadhav na pia kuangalia upya hukumu ya kifo iliyoitoa dhidi ya raia huyo wa India.
Aidha jaji Abdul Qawi Ahmad Yousuf wa Pakistan alitupilia mbali takwa la India la kumuachilia huru jasusi huyo na kisha kumrejesha nchini kwake na kuongeza kuwa hukumu hiyo haitotekelezwa hadi pale ubalozi mdogo wa India utakapofanya mawasiliano na raia wake sambamba na Islamabad nayo kutekeleza hatua nyingine za kisheria kwa ajili ya raia wa India.
Pakistan inadai kwamba Kulbhushan Jadhav ambaye ni mmoja wa maafisa wa jeshi la baharini nchini India na aliyetiwa mbaroni mwezi Machi 2016 katika jimbo la Balochistan, alikamatwa kwa tuhuma za kuifanyia ujasusi nchi yake ambapo mwaka 2017 pia alihukumiwa adhabu ya kifo na nchi hiyo. Nayo serikali ya India inadai kuwa tuhuma za ujasusi zilizoelekezwa na Pakistan kwa raia wake huyo hazina msingi wowote.
/129