5 Septemba 2019 - 15:48
 Rais Rouhani: Awamu ya tatu ya Iran kupunguza uwajibikaji katika JCPOA itaanza kesho Ijumaa

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameatangaza kuwa, awamu ya tatu ya Iran kupunguza uwajibikaji wake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA itaanza kutekelezwa kesho Ijumaa.

Rais Rouhani amesema hayo jana usiku mwishoni mwa kikao cha viongozi wa mihimili mikuu mitatu ya dola na kusisitiza kwamba, Ijumaa ya kesho ya Septemba 6 ndio siku ambayo Iran itaanza kutekeleza awamu ya tatu ya kupunguza uwajibikaji wake katika JCPOA.

Rais Rouhanii amesema, Taasisi ya Atomiki ya Iran kuanzia kesho inapaswa kuweka kando ahadi na uwajibikaji wake wote katika makubaliano ya nyuklia na kupanua utafiti na ustawi katika aina za mashinapewa mpya na kufanya urutubishaji madini ya Urani kwa kasi na kwa kadiri ya mahitaji.

Rais wa Iran amefafanua kuwa, pamoja na kuchukua hatua ya tatu, Tehran itatoa muhula mwengine wa miezi miwili kwa pande shiriki katika JCPOA; na endapo utafikiwa mwafaka, bado kuna njia ya mantiki, mazungumzo na kufikiwa makubaliano baina ya pande mbili.

Tarehe 8 Mei mwaka huu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisitisha utekelezaji wa baadhi ya majkumu yake katika makubaliano ya nyuklia kulingana na kifungu cha 26 na 36 vya makubaliano hayo. Mnamo tarehe 7 Julai, Iran ilianzisha pia mchakato wa kuvuka kiwango cha asilimia 3.67 cha urutubishaji madini ya urani katika shughuli zake za nyuklia.

.............

300