(ABNA24.com) Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Kuwait katika Umoja wa Mataifa amesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua utawala haramu wa Israel kutokana na utawala huo kufanya uvamizi huko Palestina na kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina.
Mansour Al-Otaibi, amesema hayo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha kujadili hali ya Asia Magharibi ikiwemo kadhia ya Palestina na kueleza kuwa, kutotekeleza jamii ya kimataifa majukumu yake ipasavyo ndiyo sababu ya utawala wa Kizayuni wa Israel kupata kiburi cha kuendeleza uvamizi wake, kukiuka sheria za kimataifa na kuyapa changamoto maazimio ya kimataifa.
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Kuwait katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kwa mujibu wa azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama, utawala ghasibu wa Israel unapaswa kusitisha mara moja na kikamilifu ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi unazozikalia kwa mabavu ikiwemo Quds Mashariki na kufungamana kikamilifu na sheria za kimataifa.
Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina unafanyika kwa shabaha ya kubadili muundo wa kijamii na kijiografia wa ardhi ya Palestina.
Maafisa mbalimbali wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kieneo na kimataifa ya kutetetea haki za binadamu yamekuwa yakisisitiza kwamba, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi unaofanywa na Israel katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Palestina ni kinyume cha sheria na unapaswa kusitishwa kikamilifu.
/129
22 Septemba 2019 - 06:14
Msimbo wa Habari: 977153
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Kuwait katika Umoja wa Mataifa amesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua utawala haramu wa Israel kutokana na utawala huo kufanya uvamizi huko Palestina na kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina.