(ABNA24.com) Mkutano huo wa jana ulikumbwa na mkwamo baada ya wajumbe wa pande mbili kushindwa kuafikiana kuhusu masuala yenye utata, kama suala la uwepo wa askari wa Uganda nchini Rwanda pamoja na kukamatwa kinyume cha sheria Wanyarwanda nchini Uganda.
Balozi Olivier Nduhungirehe, Waziri wa Masuala ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Rwanda amesema "Tutawashauri marais wa nchi mbili hizi, ili kujua muelekeo na msimamo juu ya mapendekezo yaliyowasilishwa. Natumai katika siku zijazo, tutakuwa na azma na irada njema ya kisiasa ya kuupatia ufumbuzi mzozo uliopo."
Hii ni katika hali ambayo, hivi karibuni nchi mbili hizo zilisisitiza umuhimu wa kufungamana na Makubaliano ya Luanda yanayozitaka nchi mbili hizo jirani zijizuie na vitendo vyovyote vya uhasama.
..........
340