30 Desemba 2019 - 07:58
Rais wa Iraq alaani mashambulio ya Marekani dhidi ya Hashd al-Shaabi; idadi ya waliouawa yaongezeka

Rais wa Iraq amelaani vikali mashambulio ya anga ya Marekani dhidi ya kambi za harakati ya wananchi ya Hashd al-Shaabi na kueleza kwamba, mashambulio hayo ni kinyume kabisa na makubaliano ya pande mbili na katu hayakubaliki.

(ABNA24.com) Rais Barham Salih amesisitiza kwamba, serikali ya Iraq inalaani vikkali mashambulio hayo ya Marekani dhidi ya kambi za Hashd al-Shaab katikak mkoa wa al-Anbar.

Ndege za kijeshi za Marekani alasiri ya jana zilishambulia kambi kadhaa za Brigedi ya Hizbullah ya harakati ya wananchi ya Hashd al-Shaabi zilizoko katika mpaka wa nchi hiyo na Syria.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon nayo imetoa taarifa na kuthibitisha kufanywa mashambulio hayo na Marekani.

Duru za harakati ya wananchi yay Hashd al-Shaabi zinasema kuwa, idadi ya waliouawa shahidi hadi sasa kufuatia mashambulio hayo imeongezeka na kufikkia mashahidi 25.

Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa, makumi ya wapiganaji wa jeshi hilo la kujitolea la wananchi wa Iraq wamejeruhiwa katika mashambulio hayo ya anga ya Marekani.

Shakhsia, viongozi, makundi na vyama mbalimbali vya kisiasa nchini Iraq vimetoa taarifa vikilaani vikali mashambulio hayo ya Marekani dhidi ya ngome za harakati hiyo inayotambuliwa kisheria nchini Iraq

Wakati huo huo, Brigedi ya Hizbullah ya Iraq, tawi la kijeshi la Harakati ya Wananchi ya Hashd al-Shaabi imesema kuwa, nguvu ya muqawama ya nchi hiyo imeongezeka mara kumi na itatoa jibu dhidi ya Marekani kkatika wakati mwafaka.

............
340