-
Hatua Tano na Muhimu Kabla ya Kuingia Katika Mjadala au Kabla ya Kufanya Mjadala na Mtu yeyote | Bila hatua hizi huo sio Mjadala Bali ni Kupoteza Muda
Kabla hujafanya mjadala wowote na mtu yeyote, unapaswa kuzingatia nukta za kimjadala na muhimu ili uepuke mapema kupoteza muda wako kwa kuingia katika mjadala usiokuwa na matunda yoyote.
-
Waliofariki dunia klabuni Jamhuri ya Dominika wafikia 218
Maafisa wa serikali katika Jamhuri ya Dominika wamesema idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mkasa wa kuporomoka kwa paa katika ukumbi wa starehe wa Jet Set katika mji mkuu Santo Domingo imepindukia 200, huku matumaini ya kupata manusura yazidi kukififia.
-
Ripota wa UN: Muda wa kuwanusuru Wapalestina unazidi kuyoyoma
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Palestina ameonya kwamba "hakuna muda mwingi uliobaki" kuwaokoa watu wa Palestina wakati huu ambapo Israel inaendeleza mashambulizi yake mtawalia katika Ukanda wa Gaza, na ukandamizaji unaoendelea katika Ukingo wa Magharibi.
-
Vita Vyenye Faida!
Tunaanza kwa swali rahisi na jepesi: Kwa nini Trump na Netanyahu hawataki kusitishwa mapigano? Na kwa nini Marekani imeanza duru mpya ya mashambulizi na hujuma kali dhidi ya Yemen sambamba na kuanza mashambulizi mapya ya Israel dhidi ya watu wa Gaza? Hebu sasa tuangalie takwimu:
-
Kusalimu amri Trump katika sera zake za vita vya kiuchumi duniani
Rais wa Marekani Donald Trump, amesalimu amri baada ya masoko ya hisa ya Marekani kuporomoka vibaya kutokana na sera zake mbovu za kuanzisha vita vya kiudhumi na kuzipandishia ushuru bidhaa za nchi zote duniani.
-
Mgawanyiko katika jeshi la Israel huku mashambulio dhidi ya Gaza yakiendelea
Kundi la askari wa akiba wa jeshi la anga la Israel limefukuzwa kazi baada ya kutia saini waraka wa kutaka kusitishwa vita dhidi ya Gaza na kurejeshwa kwa mateka wa utawala huo haramu.
-
Kimya cha dunia mkabala wa jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa Gaza imekuwa machinjioni, na zaidi ya mwezi mmoja sasa hakuna msaada wowote uliopelekwa eneo hilo na kwamba wakazi wa Gaza hawana mafuta, dawa na bidhaa nyingine zinazohitajika.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina yapongeza uamuzi wa Macron kuitambua rasmi Palestina
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imekaribisha msimamo uliotangazwa na Rais wa Ufaransa kuhusu uwezekano wa nchi hiyo kulitambua rasmi Taifa la Palestina katika miezi ijayo.
-
Mamilioni waandamana Yemen kuunga mkono Ghaza
Mamilioni ya wananchi wa Yemen wamemiminika mitaani katika mkoa wa Sa'ada leo Ijumaa na kufurika katika viwanja 35 vya mkoa huo wa kaskazini ya Yemen chini ya kaulimbiu ya "Jihadi, Uthabiti na Ushujaa... Hatutaiacha peke yake Ghaza."
-
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji: Uwezo wa kijeshi wa Iran uko juu sana
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Iran, Admeli Shahram Irani amesema uwezo na nguvu za Jeshi la Iran zimefikia viwango vya juu ambavyo havijawahi kushuhudiwa.
-
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu atahadharisha kuhusu 'hatua za kujihami' za Iran dhidi ya IAEA
Mshauri mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kwamba vitisho dhidi ya Iran vinaweza kusababisha kusimamishwa ushirikiano wa Tehran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na kufukuzwa wakaguzi wake hapa nchini.
-
Jenerali Qa'ani: Marekani, Israel 'ni dhaifu kivitendo' mbele ya Iran na Muqawama
Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kislamu nchini Iran amesema kuwa licha ya bwabwaja zao, Marekani na Israel "hazina nguvu kivitendo" dhidi ya Iran na makundi ya Muqawama.
-
Baghaei: Mazungumzo ya Jumamosi yatakuwa kipimo cha nia ya Marekani
Kwa mara nyingine tena, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani huko Muscat, mji mkuu wa Oman, ni mtihani wa kupima nia na ukweli wa madai ya Marekani.
-
Iran kwa mara nyingine yatilia mkazo wajibu wa kukomeshwa mara moja jinai Ghaza
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kuwa, kuna wajibu wa kuongezwa juhudi za kidiplomasia za kuhakikisha utawala wa Kizayuni unakomesha jinai zake kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
Ayatullah Seddiqi: Marekani haina hadhi ya kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Iran
Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa, madai ya rais wa Marekani ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Iran ni ya uongo na ya hadaa zake za kawaida na kwamba Marekani haina hadhi ya kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Iran.
-
Mahusiano ya Kijamii ya Kituo cha Utamaduni cha Iran Nchini Tanzania - Dar-es-salaam
Kituo cha Utamaduni cha Iran kipo tayari kutoa Ushirikiano katika nyanja za Utamaduni na Elimu.