Main Title

source : Parstoday
Jumatano

16 Novemba 2022

17:19:18
1323739

Donald Trump atangaza nia yake ya kugombea urais katika uchaguzi ujao 2024

Donald Trump Rais wa zamani wa Marekani aliyeshindwa na Joe Biden katika uchaguzi uliopita ametangaza nia ya kugombea urais kwa mara nyingine kupitia chama cha Republican katika uchaguzi wa 2024.

Trump ametangaza nia yake hiyo wakati kura zikiwa hazijamalizika kuhesabiwa za uchaguzi wa bunge wa katikati ya muhula wa Marekani wa 2022.

Hii itakuwa ni mara yake ya tatu kuwania, baada kumshinda mgombea wa Demokrat, Hilary Clinton mwaka 2016, na aliposhindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa 2020 baada ya kushindwa na Rais wa sasa Joe Biden.

Akiwa katika makazi yake ya Mar-a-Largo, Trump ametoa tangazo hilo huku wachambuzi wakiona ni kama kupuuzia madai ya Warepablican kwamba ni yeye aliyechangia kukosekana kwa wapiga kura wengi. 

Mpaka sasa bado analalamika kwamba uchaguzi uliopita alifanyiwa hila zilizo muwezesha rais wa sasa wa 46, Joe Biden kushinda.

Hata hivyo anakabiliwa na hali ngumu ya kisiasa licha ya kwamba kasi yake inaonekana kutozingatia hilo.

Baada ya hivi karibuni Wademokrat kupata ushindi katika uchaguzi wa Seneti na kupata wingi wa kura katika chombo hicho cha kutunga sheria nchini Marekani, Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani alitangaza kuwa: Kumefanyika udanganyifu katika duru hii ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Congress, na kwamba, wagombea wa chama cha Republican wameshindwa katika Baraza la Seneti kutokana uchakachuaji na wiziii wa kura uliofanywa na chama cha Democratic.

342/