Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

26 Novemba 2022

18:34:04
1326424

Makamu wa Rais wa Malawi atiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa

Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima amejikutan matatani baada ya kutiwa mbaroni akikabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa.

Taasisii ya kupambana na rushwa nchini Malawi imetangaza kuwa, kati ya Machi na Oktoba mwaka jana, makamu huyo wa Rais alipokea zaidi ya dola 280,000 na vitu vingine kama malipo baada ya kusaidia kampuni mbili kupewa kandarasi za serikali.

Taarifa kutoka kwa taasisi hiyo inasema Bw Chilima atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka kadhaa anayokabiliwa yakiwemo makosa matatu ya ufisadi.

Chilima aligombea kiti cha urais mwaka 2019 lakini akashika nafasi ya tatu katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali nchini Malawi. 

Baadaye mwanasiasa huyo aliungana na Rais wa sasa Lazarus Chakwera katika kama mgombea mwenza. Hata hiivyo uhusiano wa hivi karibuni kati ya Makamu wa Rais na Rais Chakwera umezorota kutokana na shutuma za ufisadi na upendeleo serikalini zinazomuandama mshirika wake huyo wa kisiasa

Saulos Chilima amewahi kufanya kampeni kubwa na kutangaza sera yake ya kupinga ufisadi akiahidi kumaliza miongo kadhaa ya ufisadi uliokita mizizi serikalini sambamba na kutokomeza umaskini mkubwa nchini Malawi ambayo ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani.

Itakumbukwa kuwa nchi hiyo ya kusini mwa bara la Afrika inategemea pakubwa misaada ya nchi wafadhili na imekumbwa na ukame mkubwa mara kadhaa na  kuwaathiri mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo.

342/