Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

26 Januari 2024

15:51:52
1432564

Hatima ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya jinai za Israel huko Gaza kujulikana Ijumaa hii

Ijumaa ya tarehe 26 mwezi huu wa Januari mwaka 2024 huko The Hague, Uholanzi, Mahakama ya Kimataifa ya Haki inatoa uamuzi juu ya shauri la Afrika Kusini la kuitaka itoe agizo juu ya ombi lake la kutaka ichukue hatua za awali dhidi ya utawala wa Kizayuni Israel kutokana na mauaji yake ya kimbari huko Gaza dhidi ya Wapalestina.

Uamuzi huo unaotarajiwa Ijumaa unafuatia Mahakama hiyo kusikiliza kwa siku mbili upande wa mlalamikaji Afrika Kusini na mlalamikiwa Israeli ambapo Afrika Kusini inataka kile kinachofanywa na Israeli huko Gaza dhidi ya wapalestina kitambuliwe kuwa ni Uhalifu wa mauaji ya kimbari kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa wa kuzuia na kuadhibiti uhalifu wa maujaji ya kimbari wa mwaka 1948.

Kwa mujibu wa taarifa ya ICJ, Afrika Kusini imependekeza hatua za muda ili kuepusha madhara zaidi na kulinda haki za wananchi wa Palestina kwa mujibu wa Mkataba huo wa huo na vile vile kuhakikisha Israeli inazingatia Mkataba kwa kuwa ni mwanachama.

Mathalni Israel isitishe mara moja operesheni zake za kijeshi ndani na dhidi ya Gaza na vile vile serikali hiyo ya Israeli ihakikishe vikosi vyake vya kijeshi vilivyo rasmi na visivyo rasmi haviendelezi operesheni hizo ndani na dhidi ya Gaza.Israeli pia ichukue hatua za kimsingi kuepusha mauaji ya kimbari. Pia ichukue hatua zote ndani ya uwezo wake kufuta amri zinazohusiana na mashambulizi ikiwemo za kuzuia au kufukuza na kufurusha watu kutoka makazi yao; Watu kunyimwa fursa ya kupata chakula cha kutosha na maji.

Hatua nyingine ni serikali ya Israeli  ichukua hatua fanisi kuzuia uharibifu na ihakikishe ushahidi wowote kuhusiana na uharibifu wowote unahifadhiwa.

Hatua za awali ni aina ya zuio la muda. Lengo lake ni kusitisha kwa muda hali inayoendelea hadi pale Mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho kuhusu mzozo unaoendelea.

Wakati huo huo, taarifa ya mashirika ya kimataifa inasema, vita vya uharibifu vya Israel dhidi ya watu wa Gaza vimesababisha uharibifu wa 75% ya shule katika ukanda huo.

Wizara ya Afya ya Palestina ilitangaza jana kuwa, idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia 25,700 na idadi ya waliojeruhiwa ni 63,740.342/