Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

7 Juni 2024

15:09:24
1463968

Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Israel imo kwenye maangamizi

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa imeonyesha udhaifu halisi wa utawala wa Kizayuni na imekuwa utangulizi wa kuangamizwa utawala huo.

Hujjatul-Islam Kazem Seddiqi ameelezea vipengele mbalimbali vya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na athari zake katika kuporomoka kwa haiba bandia ya utawala haramu wa Kizayuni na kufeli kwa mpango wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala huo na baadhi ya nchi na akasema: Kimbunga cha Al-Aqsa kiliitokomeza moja kwa moja na kuifanya isiweze kufufuliwa njama ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida. Hujjatul-Islam Seddiqi ameendelea kueleza kwamba: Kimbunga cha Al-Aqsa kilitoa kipigo kisichoweza kurekebishwa kwa shina la demokrasia ya kiliberali ya Magharibi na mtoto wake wa haramu utawala wa Kizayuni, ambapo kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo wa Magharibi, leo hii Uzayuni unaendelea kuyeyuka na kutoweka.

Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria mambo matatu aliyozungumzia Imam Khomeini (MA) kuhusiana na kutokomezwa utawala wa kifalme na udikteta, kukabiliana na Uzayuni na unyonyaji, na hatimaye mapambano dhidi ya Marekani na kambi ya vita dhidi ya Uistikbari na akasema: Imam Khomeini (MA) aliligeuza suala la Palestina na mapambano dhidi ya Israel kuwa suala la Ulimwengu wa Kiislamu.

 Imamu wa Muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amezungumzia pia operesheni ya Ahadi ya Kweli ya Iran ya kuutia adabu utawala wa Kizayuni na kuitaja kuwa ustadi mkubwa uliofanywa na vijana wa Imam Khomeini (MA) na Mapinduzi ya Kiislamu na Walinzi walio weledi wa nyakati ambao waliigeuza mbinu ya ulinzi kuwa mbinu ya kuzuia hujuma na ya mashambulizi. Katika sehemu nyingine ya hotuba hiyo ya Sala ya Ijumaa, Hujjatul-Islam Seddiqi ameashiria pia duru ya 14 ya uchaguzi wa rais wa Iran na kuelezea baadhi ya vipengele vya sifa za uchaguaji kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na akasema: njia ya Rais aliyekufa shahidi, Sayyid Ebrahim Raisi inapasa iendelezwe...

342/