Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:18:00
1471083

Trump amwalika tena Biden kufanya mdahalo mwingine wiki hii

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amemwalika mpinzani wake katika uchaguzi, Rais aliyeko madarakani Joe Biden, kufanya mdahalo mwingine wiki hii kama fursa ya "kujiokoa" baada ya utendaji mbaya wa hivi majuzi aliounyesha katika mdahalo huo.

Katika matamshi yake Trump amesema; "Ninampa Joe Biden rasmi nafasi ya kujikomboa mbele ya ulimwengu mzima," Rais huyo wa zamani Donald Trump alisema katika mkutano wa hadhara huko Florida.

Trump alisema kwamba; Wacha tufanye mdahalo mwingine wiki hii ili Joe Biden aliye na usingizi aweze kuthibitisha kwa kila mtu duniani kote kwamba ana kile kinachohitajika kuwa rais tena na kuweza kuongoza wananchi wa Marekani," rais huyo wa zamani wa Marekani alisisitiza.

Hata hivyo Donald Trump, alisema mara hii mdahalo unapaswa kuwa  wa ana kwa ana, hakuna wasimamizi, hakuna kusimamishwa na kuzuiliwa.Mnamo Juni 27, 2024 mwaka huu Atlanta iliandaa mdahalo wa kwanza kabisa wa uchaguzi wa televisheni kati ya rais Joe Biden anayeshikilia madaraka hivi sasa huko nchi Marekani na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika historia ya Marekani. Uchaguzi wa Rais nchini Marekani umepangwa kuufanyika mnamo Novemba 5, mwaka huu (2024, Trump tayari amepata idadi muhimu ya kura za awali ili kuwania uteuzi wa chama cha Republican. Na rais Joe Biden, anayewania kuchaguliwa tena, alishinda mchujo katika chama chake cha Democrats huko New Jersey na Washington, DC, katika baadhi ya mashindano ya mwisho mwezi Juni uliopita mwaka huu.

342/