Wanadiplomasia hao wawili walifanya mazungumzo katika mji mkuu Tehran siku ya Jumapili ili kujadili kushadidi mvutano katika eneo pamoja na uhusiano wa pande mbili.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan ilisema katika taarifa mapema Jumamosi kwamba Safadi pia ana ujumbe kutoka kwa Mfalme Abdullah II kwa rais wa Iran kuhusu "hali katika eneo na uhusiano wa pande mbili."
Ziara hiyo ya nadra ya waziri wa mambo ya nje wa Jordan inakuja siku moja baada ya mazungumzo yake ya simu na mawaziri wenzake wa Iran na Misri kuhusu hatua ya utawala wa haramu wa Israel ya kumuua kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran.
Bagheri Kani ameandika katika chapisho kwenye akaunti yake ya X kwamba wakati wa mazungumo hayo ya simu, mawaziri hao watatu wa mambo ya nje walibadilishana mawazo kuhusu matukio ya eneo, akibainisha kuwa "walisisitiza kuendelea kwa mashauriano kati ya nchi za eneo."
Ameendelea kusema hali ya eneo la Asia Magharibi ni nyeti sana kutokana na kuendelea jinai za Wazayuni.
342/