Main Title

source : Parstoday
Jumanne

6 Agosti 2024

15:10:54
1477033

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Ni lazima tusimame dhidi ya utawala mshari wa Kizayuni

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Tehran inapaswa kusimama kidete kukabiliana na utawala muovu kwa jina la utawala wa Kizayuni, ambao ndio chanzo cha ukosefu wa amani katika eneo.

Ali Bagheri Kani jana usiku alizungumza kwa simu na Peter Ciarto, Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary ambaye nchi yake pia ni mwenyekiti wa kiduru wa Umoja wa Ulaya kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na utulivu katika eneo la Asia Magharibi, kulaani hujuma za utawala wa Kizayuni za kukiuka kanuni za haki za kimatiafa na haki ya kisheria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kulinda usalama, mamlaka ya kitaifa na umoja wa ardhi nzima ya nchi hii. 

Bagheri Kani ameongeza kuwa, ukitupia macho rekodi za mashambulizi ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza utaoona kuwa utawala huo kwa kiasi kikubwa umeshambulia maeneo ya raia, hospitali, nyumba za raia, watoto,  wanawake na watu wasio na ulinzi. 

Mkuu wa chombo cha diplomasia wa Iran ameashiria kuuliwa kigaidi Ismail Haniyeh Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestinan (Hamas) hapa Tehran na kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Wazayuni hivi karibuni ni ukiukaji wa usalama, mamlaka ya kitaifa ya Iran, amani na uthabiti wa eneo; na ndio maana hatua yao hiyo inahesabiwa kuwa tishio dhidi ya amani na usalama wa dunia. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa hatua mkabala inapasa kuchukuliwa dhidi ya hujuma hiyo ya Wazayuni.  Katika mazungumzo hayo ya simu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary amesema kuwa nchi yake ina hamu na iko tayari kuendeleza mazungumzo na Iran na kusisitiza kuwa Hungary ina wasiwasi kuhusu kushtadi mivutano magharibi mwa Asia. Amesema, jamii ya kimataifa inapasa kuchukua hatua ili kuzuia kuongezeka mivutano katika eneo.  


342/