Sikumoja Imam Jaafar Swadiq a.s alikwenda kwenye kikao cha Mansuri, ambapo alimkuta Mansuri akiwa na muhindi ambaye alikuwa ni mganga na alikuwa akitalii na kuisoma vitabu vya uganga, na Imam Jaafar Swadiq a.s alisukuti kimya wakati Muhindi akisoma, alipomaliza Muhindi akamuuliza Imam Jaafar Swadiq a.s. Je unahitaji msaada wowote?,
akamjibu hapana, nilichokuwa nacho ni bora kuliko ulicho kuwanacho, akamuuliza nikipi hicho?, Imam Jaafar Swadiq a.s akajibu: Natibu ya joto kwa baridi na ya baridi kwa joto, na ya unyevu kwa makavu na makavu kwa ya unyevu, na mambo yote yanarudi kwa Mungu mtukufu, na pia natibu kwa kutumia mafunzo ya Mtume Muhammad s.a.w . ambaye alieleza kuwa utumbo ndio sehemu kunakokusanyika maradhi na kifuko cha kusaga chakula ndio tiba na mwili utarejea katika mazoea yake.
Muhindi akamuuliza ni hayo tu au kuna lingine jipya?!, Imam jaafar swaadiq [a.s.] akamuuliza unadhani haya nimeyapata kutoka kwenye vitabu vya uganga?, Muhindi akajibu ndio, Imam Jaafar Swadiq a.s akamwambia: sivyo wallahi mimi nimechukua kutoka kwa Mungu alie takasika, sasa niambie, Je wewe ni mganga mkuu au mimi?,
Muhindi; alimjibu mimi ndio mkuu na mjuzi zaidi., Imamu Jaafar swaadiq [a.s.] akamwambia sasa nakuuliza kidogo,Muhindi akasema uliza,
Imam Jaafar Swadiq a.s akauliza ewe Muhindi kwanini katika kichwa kuna vitu vingi?,Mhindi akajibu: sijui, Imam Jaafar Swadiq a.s akamuuliza: kwanini nywere ziwe juu ya kichwa?, akajibu sijui, , akamwuliza, Kwanini paji la uso liwe karibu na nywele?, akajibu sijui, Imam Jaafar Swadiq a.s akamuuliza, kwanini Paji lina misitari na mikunjo?, akajibu sijui. Akamuuliza kwanini Nyusi zipo juu ya macho?, akajibu sijui. Imam Jaafar Swadiq a.s akamuliza, kwanini macho yamekuwa duara kama goroli?, akajibu sijui. Akauliza kwanini pua ikawa kati ya macho?, akajibu sijui. Akamuuliza kwanini matundu ya pua yameangalia chini?, akajibu sijui, Akauliza kwanini mdomo unavipande viwili na kunywa au kula iwe katiyake?, akajibu sijui. Imam Jaafar Swadiq a.s akamuuliza, kwanini meno ya mbele membamba na yakutafunia manene na yakukamatia marefu?, akajibu sijui. Akauliza kwanini ndevu imekuwa kwa wanaume tu ?, Akajibu sijui. Imam Jaafar Swadiq a.s akauliza kwanini vitangaja vya mikono havina nywele?, Akajibu sijui, kwanini nywele na kucha hazina uhai?, Akajibu sijui. Imam Jaafar Swadiq a.s, akauliza, kwanini moyo uko kama tunda lenye mishipa?, Mhindi akajibu sijui. Akauliza kwanini mapafu yapo vipande viwili na je lenyewe ndio sababu ya kutingishika ?, akajibu sijui. Akauliza kwanini moyo upo kama udongo?, akajibu sijui, Akauliza kwanini figo kamatunda liloshikana kwa kamba yake?, akajibu sijui, Akauliza kwanini mishipa ya shingo ipo kwa nyuma?, Akajibu sijui, Akauliza kwanini nyayo ipo batabata?, Mhindi akajibu sijui,
Imam Jaafar Swadiq a.s akamwambia; mimi najua majibu ya maswali haya.
Mhindi akamwambia nifahamishe majibu yake,
Imam Jaafar Swadiq a.s akamwambia: kwenye kichwa kimekuwa na mambo mengi kwasababu kichwa bila ya kuwa na mambo mengi, ingesababisha kuwepo kwa maradhi ya kichwa, kwakuwepo mambo mengi imekuwa sababu ya kukosekana maradhi hayo, ameziweka nywele juu ya kichwa ili ifikishwe hewa kwenye ubongo na zipitishe jasho ili ubongo upate hewa na baridi, na paji la uso limekosa nywele kwakuwa nuru inayo piga hapo hung’arisha macho, na imekuwa na mistali na mikunjo ili iziwie jasho litalo tiririka kutokea kichwani lisiingie kwenye macho moja kwa moja, linase kwenye mistali na mikunjo hiyo, nisawa na mvua maji yake yanakwama kwenye ardhi yenye matuta, ameweka nyusi juu ya macho ili izuie kasi ya nuru na mwanga ili ifike ule unayo hitajika, hivi huoni ewe Muhindi anae zidiwa na nuru huweka mikono yake juu ya macho yake ili kusawazisha mwanga ufike kadiri na kiwango kinachotakiwa?, akaifanya pua iwe kati ya macho ili mwanga ugawike kwenye macho mawili ili kilajicho lipate mwanga kwa usawa, macho yamekuwa ya duara ili yanapo zunguka yawe kwa usalama na yanatoa uchafu [tongotongo] kama yangekuwa ya pembe nne au ya mzunguko yasingeweza kugeuka kwa urahisi wala uchafu usinge toka, na tundu za pua zimetazamia chini kwa ili yatoe makamasi yatokayo kwenye ubongo na uchafu mwengine na ivute hewa safi kwenda kwenye mapafu, laiti ingeangalia juu isinge penga makamasi wala kupumuwa hewa safi, kinjwa kumekuwa kati ya vipande viwili vya mdomo ili kuzuia makamasi na koozi ili yasichanganyike na chakula na kinjwaji cha binaadamu na kukitumia mwenyewe. Ndevu wamepewa wanaume ili aeleweke machoni mwa watu yupi mwanaume? Na yupi mwanamke, ameyafanya meno ya mbele makali ili yakate chakula na yapembeni kuwa mapana ili yasage na kulainisha chakula na meno manne malefu kwa ajili ya kurarua na kukamata chakula kigumu na ninguzo kati ya meno ya kukata na kusaga, vitangaja vimekosa nywele kwakuwa hizo ni sehemu ya hisia, laiti ingekuwemo nywele mwanaadamu asingeweza kufahamu ni kitu gani anacho kigusa, kucha na nywele zimekosa uhai kwakuwa kilicho refuka ni uchafu uchukizao na kuikata kwake ni vizuri, laiti vingekuwa na uhai mwanaadamu angaliumia wakati wa kukata nywele na kucha, na moyo kama tunda na kichwa chake laini ili damu iingie na unadunda ili kusukuma damu na kuizuia isigande, Mapafu yamekuwa na vipande viwili ili hewa iingie sehemu zote ili zicheze kwa msukumo wake, na maini yamekuwa mazito kama udongo ili itie uzito kwa kutuliza msukumo wake, kwa kujikamua na kutoa jasho, na figo imekuwa ya duala na kamba za kuniginia kwasababu ndio njia ya manii laiti ingekuwa yenye pembe nne au yakujizinga manii yangalitoka maramoja na raha ya kutoa mbegu isinge kuwepo, kwahiyo manii yanatoka ndani ya uti wa mgongo mpaka kwenye peke inazoa mbegu kama vijududu na kupitia kwenye figo kama urojo. Mishipa ya shingo aliiweka nyuma kwa kuwa mtu anatembea akiwa sawa wa mwendo wake laiti sihivyo angalianguka wakati wa kutembea, na nyayo imewekwa batabata kwakuwa kitu kikianguka chote aridhini kinakuwa kizito kama jiwe na akiwa upande mmoja kabeba mtoto nivigumu kuinuka kwa miguu yake,
Muhindi akamuuliza nani kakufundisha elimu hio?, Imamu Jaafari Saadiq [a.s.] akajibu: nimeelimishwa kutoka kwa wazazi wangu kutoka kwa Mtume [s.a.w.w.] kutoka kwa Jibril [a.s.] kutoka kwa Mwenyezi Mungu alie takasika ambae ameumba miili na roho.
Muhindi akasema uliosema ni kweli na mimi ninashuhudia kuwa hakuna miungu ila Mwenyezi Mungu mmoja na Muhammad ni Mtume wa Mungu na mja wake.
source : abna.ir
Alhamisi
2 Oktoba 2014
18:47:50
641913
Ni kisa cha Imamu Jaafar Swadiq alipokutana na Mganga wa kihindi, na kujiri mazungumzo yenye mafunzo ya ajabu kutoka kwa Imam Jaafar Swadiq ambayo yalimstaajabisha Mhindi huyo.