Main Title

source : Pars Today
Jumatano

26 Juni 2019

08:52:20
955223

Jumuiya ya waandishi magazeti wa Kiarabu yalalamikia kualikwa vyombo vya habari vya Kizayuni huko Bahrain

Jumuiya ya waandishi wa magazeti wa Kiarabu imelalamikia vikali hatua ya kualikwa vyombo vya habari vya Kizayuni kuakisi mkutano ulio dhidi ya Wapalestina wa mjini Manama Bahrain.

(ABNA24.com) Jumuiya ya waandishi wa magazeti wa Kiarabu imelalamikia vikali hatua ya kualikwa vyombo vya habari vya Kizayuni kuakisi mkutano ulio dhidi ya Wapalestina wa mjini Manama Bahrain.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Anatoli la nchini Uturuki, jumuiya hiyo ya waandishi wa magazeti wa Kiarabu imetoa taarifa ikielezea wsiwasi wake kuhusiana na hatua hiyo ya kualikwa vyombo vya habari vya Kizayuni katika mkutano huo unaotazamiwa kuanza leo huko Manama, mji mkuu wa Bahrain.

Jumuiya hiyo imesema kuwa iko bega kwa bega na watu wa Palestina katika kutetea haki zao za msingi na kusimama kidete dhidi ya njama hatari za Wamarekani na Wazayuni dhidi ya taifa la Palestina kupitia kongamano la Manama lililopewa jina la 'Muamala wa Karne.'

Jumuiya hiyo ya waandishi wa magazeti wa Kiarabu inasema kuhudhuria vyombo vya habari vya Kizayuni kongamano hilo la Bahrain kunapingana moja kwa moja na misingi ya jumuiya hiyo ambayo inapinga kila aina ya uboreshaji uhusiano na utawala haramu wa Israel. Imevitaka vyombo vya habari vya Kiarabu kuviwekea vikwazo na kutoshirikiana kwa njia yoyote ile na vyombo hivyo vya habari vya Kizayuni ambavyo vina lengo la kupenya katika nchi za Kiislamu na Kiarabu kwa madhumuni ya kupoteza na kufunika haki za msingi za taifa madhukumu la Palestina.

Kongomano la Manama ambalo limepewa jina la 'Muamala wa Karne' limepangwa na kusimamiwa na Marekani, utawala haramu wa Israel na baadhi ya nchi vibaraka za Kiarabu na limepangwa kuanza leo Jumanne na kumalizika kesho Jumatano.




/129