(ABNA24.com) Katika barua yao kwa ofisi yya Umoja wa Mataifa na ubalozi wa Nigeria hapa mjini Tehran, Chama cha Wahadhiri na Wanachuo wa Sayansi ya Tiba nchini Iran kimetaka kuachiliwa huru haraka Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusiana na hali ya kiafya ya kiongozi huyo wa harakati ya Kiislamu nchini Nigeria.
Kadhalika Chama cha Wahadhiri na Wanachuo wa Sayansi ya Tiba nchini Iran kimewataka maulama wa Kiislamu, wanaharakati wa masuala ya kiutamaduni na wa haki za binadamu kufuatilia kwa karibu hali ya matibabu ya Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, jana Sheikh Muhammad Jafar Montazeri Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwaandikia barua viongozi wa vyyombo vya mahakama vya Nigeria akilaani vikali hatua ya wanajeshi wa Nigeria dhidi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, na kutoa wito wa kuachiliwa huru mwanazuoni huyo na kuletwa hapa Iran kwa ajili ya matibabu.
Mwaka 2015, jeshi la Nigeria lilivamia na kushambulia mkusanyiko wa Waislamu katika Husseiniyah ya Baqiyatullah huko Zaria kwenye jimbo la Kano na kuua shahidi kwa umati karibu Waislamu elfu moja.
Sheikh Zakzaky mwenyewe na mkewe walipigwa risasi na tangu wakati huo wanashikiliwa katika korokoro za serikali ya Rais Muhammadu Buhari ambayo inaendelea kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya kumwachilia huru mwanachuoni huyo.
/129
22 Julai 2019 - 06:05
News ID: 963356

Chama cha Wahadhiri na Wanachuo wa Sayansi ya Tiba nchini Iran kimetahadharisha kuhusiana na hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.