Mohsen Rezaei
-
Mohsen Rezaei: Madai ya njama ya Iran kumuua mtoto wa Trump ni propaganda za uongo za Netanyahu
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Meja Jenerali Mohsen Rezaei, amekanusha madai ya kuwepo kwa njama ya Iran ya kumuua mtoto wa Trump, akiyataja kuwa ni propaganda zilizobuniwa na hila za Benjamin Netanyahu.
-
Mohsen Rezaei: Marekani ikichukua hatua ya uhasama dhidi ya Iran, tutalenga maslahi yake kwa namna itakayorekodiwa katika historia
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Meja Jenerali Mohsen Rezaei, ameonya kuwa iwapo Marekani itachukua hatua yoyote ya uhasama dhidi ya Iran, Tehran itachukua hatua dhidi ya maslahi yake ya kijeshi na kiuchumi kwa namna itakayorekodiwa katika historia.
-
Rezaei: Marekani Ichukue Hatua za Vitendo Kutekeleza Masharti ya Mkataba wa Makubaliano
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Meja Jenerali Mohsen Rezaei, amesema Marekani inapaswa kubadili mwenendo wake na kuchukua hatua za vitendo kutekeleza masharti yaliyowekwa katika Mkataba wa Makubaliano, huku akisisitiza kuwa Iran haisadiki Marekani.
-
Mohsen Rezaei: Nchi yoyote itakayounga mkono vita vya kiuchumi dhidi ya Iran tutachukulia hatua hiyo kuwa kitendo cha kivita
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Meja Jenerali Mohsen Rezaei, ameonya kuwa Iran itachukulia ushiriki au uungaji mkono wa nchi yoyote katika kile alichokiita vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya wananchi wa Iran kuwa “kitendo cha kivita.”
-
Mohsen Rezaei: Mlango wa Hormuz Hautafunguliwa Bila Kusitishwa kwa Vita Gaza na Lebanon
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, amesema Mlango wa Hormuz hautafunguliwa hadi Marekani ikubali kusitishwa kwa mapigano katika maeneo ya Gaza na Lebanon pia.
-
Waziri wa Mambo ya Ndani Pakistan: Uhusiano Imara wa Tehran na Islamabad Ugeuzwe Kuwa Matokeo ya Kivitendo
Mohsin Naqvi amesema uhusiano wa kina kati ya wananchi wa Iran na Pakistan unapaswa kuzaa ushirikiano zaidi na matokeo ya kivitendo, akisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za pamoja katika kufikia malengo ya nchi hizo mbili.
-
Rais Pezeshkian Amteua Mohsen Rezaei kuwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amemteua Mohsen Rezaei kuwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, akimtaka kuimarisha uratibu wa taasisi za usalama, kukabiliana na vitisho vipya na vya kiteknolojia, na kulinda umoja wa kitaifa, mamlaka na uadilifu wa ardhi ya Iran.
-
Kaimu Waziri wa Ulinzi: Uwepo wa viongozi wenye uzoefu katika nafasi za kimkakati ni faida kwa kulinda maslahi ya taifa
Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Majid Ibn al-Reza, amempongeza Meja Jenerali Mohsen Rezaei kwa kuteuliwa kuwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, akisema uwepo wa watu wenye imani, uzoefu, uelewa na historia ya kujitolea katika nafasi za kimkakati ni rasilimali muhimu kwa kulinda maslahi ya kitaifa na kuimarisha nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Ejei kwa Katibu mpya wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa: Kulitumikia taifa la Kiislamu ni wajibu wa lazima
Mkuu wa Mamlaka ya Mahakama ya Iran, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Gholam-Hossein Mohseni Ejei, amempongeza Mohsen Rezaei kwa kuteuliwa kuwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, akisisitiza kuwa kulitumikia taifa la Kiislamu ni wajibu wa lazima, hasa katika kukabiliana na njama zinazolenga kuidhoofisha Iran na mfumo wake.
-
Meja Jenerali Abdollahi: Uwepo wa Rezaei katika Baraza la Usalama wa Taifa utaimarisha uratibu kati ya uwanja wa vita na diplomasia
Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya, Meja Jenerali Ali Abdollahi, amesema uwepo wa Mohsen Rezaei katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika uratibu wa kimkakati kati ya shughuli za uwanjani na diplomasia, pamoja na masuala ya kiusalama, kiuchumi na kisiasa.
-
Kamanda Hatami: Uzoefu wa Mohsen Rezaei ni nyongeza muhimu katika Sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amempongeza Meja Jenerali Mohsen Rezaei kwa kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na kuwa Katibu wake, akisema uzoefu na ujuzi wake katika masuala ya usalama wa taifa na kimkakati ni rasilimali muhimu kwa baraza hilo.
-
Jenerali Mohsen Rezaei: Jibu kwa ukiukaji wowote wa hati ya maelewano litakuwa la haraka na lenye nguvu
Kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Jenerali Mohsen Rezaei, amesema kuwa Iran itajibu kwa haraka na kwa nguvu ukiukaji wowote wa hati ya maelewano, akiishutumu Marekani kwa kukiuka baadhi ya vipengele vya makubaliano hayo kupitia kuunga mkono makundi washirika wake katika eneo na kuendelea kuchochea mvutano katika Mlango wa Hormuz.
-
Mohsen Rezaei: Mashambulizi dhidi ya Iran yamejibiwa, hatua mpya zitakabiliwa na majibu makali zaidi
Mohsen Rezaei amesema kuwa wale waliofanya mashambulizi dhidi ya Iran tayari wamepata majibu yao, akionya kuwa hatua yoyote mpya ya uchokozi itajibiwa kwa nguvu zaidi na gharama kubwa kwa wavamizi.