mapigano
-
Qatar: Marekani imeiomba Dola kuwasiliana na Iran ili kuiomba ikubali kusitisha mashambulizi na kumaliza vita na Israel
Washington imeiomba Qatar kuwasiliana na Iran ili kujua jinsi Iran ilivyokuwa tayari kusitisha mapigano na Israel.
-
Hasira ya Lieberman kwa kushindwa kwa Israel kufikia malengo yake maovu
Hili la kusitisha mapigano ni la aibu, si mpango wa makombora wa Iran umeharibiwa wala mpango wao wa nyuklia, huu ni usitishaji mapigano usio na masharti, Iran itarutubisha Uranium (ya Nyuklia) tena.
-
India na Pakistan Wakubaliana Kuwarudisha Wanajeshi katika Mipaka ya Awali Kabla ya Mvutano wa Kijeshi
New Delhi na Islamabad Wakubaliana Kuwarejesha Wanajeshi wao katika Nafasi za Kabla ya Mapigano. India na Pakistan wamefikia makubaliano ya kijeshi ya kurejesha vikosi vyao katika mojawapo ya maeneo ya mpaka yaliyokuwa na mvutano, hali ambayo ilizidi kuwa mbaya baada ya shambulio la kigaidi la tarehe 22 Aprili huko Kashmir. Makubaliano haya yamefikiwa baada ya kuongezeka kwa mivutano na mashambulizi ya kuvukiana mipaka, na yanakusudia kupunguza hali ya hatari ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili. Kwa mujibu wa taarifa rasmi, urejeshaji wa wanajeshi kwenye nafasi za awali unatarajiwa kukamilika kufikia mwisho wa mwezi Mei.
-
Dola bilioni 8: Gharama ya kashfa (fedheha) na mashambulizi yaliyoshindwa ya Marekani nchini Yemen
Vyombo vya habari vya Marekani vimekadiria gharama ya mashambulizi ya nchi hiyo dhidi ya Yemen, katika muktadha wa kuunga mkono Israel, kufikia dola bilioni 8. Vimeripoti kuwa Trump alikuwa akimkejeli Biden kwa sababu ya gharama za vita dhidi ya Yemen, lakini yeye mwenyewe alisababisha hasara kubwa zaidi, huku Serikali ikificha takwimu halisi za vifo.
-
Watu 5 Wauawa Katika Shambulio la Mizinga la Jeshi la India katika eneo la Kashmir
Watu 5 Wasio Wanajeshi, Wakiwemo Mtoto Mmoja, Wauawa Katika Shambulio la Mizinga la Jeshi la India Katika Eneo la Kashmir Linalodhibitiwa na Pakistan.