25 Aprili 2020 - 08:00
Haniya na Abbas wasisitiza: Taifa la Palestina litakabiliana kwa umoja wake na mpango wa Marekani wa "Muamala wa Karne"

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wamesisitiza kuwa taifa la Palestina litakabiliana kwa umoja wake na mpango wa Marekani wa Muamala wa Karne.

(ABNA24.com) Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Ismail Haniya, Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas wamebadilishana mawazo katika mazungumzo waliyofanya kwa njia ya simu kuhusu matukio ya kisiasa yanayojiri katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, likiwemo la kuundwa serikali mpya ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambayo imepanga kutekeleza mpango wa Muamala wa Karne kwa kulipora na kuliunganisha eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi za Palestina zilizopewa jina la Israel.

Katika mazungumzo hayo, Haniya ameeleza kwamba, wananchi wa Palestina hawataukubali mpango wowote ambao lengo lake ni kulipora haki za taifa la Palestina.

Itakumbukwa kuwa Januari 28 mwaka huu, Rais Donald Trump wa Marekani, akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu alizindua mpango wa kidhalimu na kibaguzi wa "Muamala wa Karne" katika Ikulu ya White House.

Miongoni mwa vipengee muhimu zaidi vya mpango huo wa unyongeshaji na udhalilishaji ni kutambuliwa rasmi Baitul Muqaddas (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, kumilikishwa utawala huo wa Kizayuni asilimia 30 ya ardhi ya Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, kufutwa moja kwa moja haki ya wakimbizi Wapalestina kurejea kwenye nchi yao na kupokonywa silaha kikamilifu kile kitakachojulikana kama nchi ya Palestina.

.............
340