(ABNA24.com) Sadeq al Husseini ameongeza kuwa, hadi sasa magaidi hao hawajaweza kufanikiwa kutekeleza lengo lao kuu nchini Iraq. Hali kadhalika afisa huyo wa Al-Hashd Al-Shaabi amebaini kuwa magaidi waliosalia wa ISIS wanahusika katika ongezeko la hujuma za kigaidi mkoani Diyala na mikoa mingine ya Iraq.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano katika Harakati ya Al-Hashd Al-Shaabi katika mkoa wa Diyala mashariki mwa Iraq ameikosoa vikali Marekani kwa kuwapa himaya ya kilojistiki magaidi wa ISIS ikiwa ni pamoja na kuwasafirisha na kuongeza kuwa: "Baada ya Bunge la Iraq kupitisha muswada wa kutaka wanajeshi wa kigeni waondoke Iraq, hivi sasa vibaraka wa Marekani wanatekeleza njama maalumu ya kuvuruga usalama wa Iraq."
Katika kipindi cha siku chache zilizopita wapiganaji wa jeshi la kujitolea la wananchi la Al-Hashd Al-Shaabi walitekeleza oparesheni kadhaa katika mkoa wa mpakani wa Diyala kwa lengo la kuwatimua na kuwaangamiza magaidi wa ISIS waliokuwa wamesalia eneo hilo.
..............
340