(ABNA24.com) Rais Rouhani amesema hayo leo Jumapili katika kikao cha Kamati ya Taifa ya Kupambana na Corona na kuongeza kuwa, kulingana na vielelezo na maamuzi ya kiafya, kwa mfano kama maambukizi ya corona yatakuwa ni sifuri kwa muda wa wiki moja katika mji fulani na ukawa hakuna mtu aliyefariki dunia kwa corona katika kipindi hicho na idadi ya waliopata afueni ikawa imeongezeka na hali hiyo ikaendelea pia katika wiki ya pili, Wizara ya Afya ya Iran inalitambua eneo hilo kuwa ni jeupe.
Amefafanua zaidi kwa kusema, katika eneo lolote lile humu nchini ambalo litakuwa limetimiza masharti ya kuitwa eneo jeupe na jambo hilo kuthibitishwa na Wizara ya Afya, basi serikali itayafungua maeneo ya ibada kwenye eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema pia kuwa, kwa mujibu wa Wizara ya Afya, hadi hivi sasa karibu miji 127 imetangazwa kuwa ni sehemu nyeupe nchini Iran hivyo maeneo matukufu na ya ibada katika sehemu hizo yatafunguliwa kwa taarifa rasmi kutoka Wizara ya Afya.
Amezungumzia pia jinsi Iran ilivyoweza kujitosheleza hivi sasa katika uzalishaji wa vifaa vya tiba na matibabu na kuongeza kuwa, maadui wamehamaki sana kuona mafanikio hayo makubwa ya Iran licha ya kuwa nchi hii iko chini ya mashinikizo makubwa ambayo maadui walidhani yataliangamiza kabisa taifa la Iran.
.............
340