Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Rouhani ameyasema hayo baada ya muswada uliopendekezwa na Marekani katika Baraza la Usalama la UN kwa ajili ya kurefusha muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran kuambulia kura mbili tu za ndio, mbili za kuupinga na wanachama wengine 11 wamejizuia kupiga kura. Nchi mbili wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama yaani China na Russia zimeupinga muswada huo kuwa kupiga kura ya hapana.
Akihutubia kikao cha Tume ya Taifa ya Kupambana na Corona mapema leo, Rais Rouhani amesema kuwa kushindwa Marekani katika kikao cha jana cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutabakia hai katika historia ya mapambano ya Iran dhidi ya ubeberu. Ameongeza kuwa, sababu ya kushindwa muswada huo wa Marekani kwa ajili ya kurefusha muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran ni kwamba kulindwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni muhimu na jambo la dharura kwa maslahi ya kikanda na kimataifa.
Rais Rouhani amesema Wamarekani wametaka kuficha fedheha hiyo ya kushindwa kwa kutangaza kuwa wametwaa meli nne za Iran na kuongeza kuwa: Marekani imetoa madai hayo ilhali meli hizo na hata bendera zake hazikuwa za Iran; na madai hayo yametolewa kwa shabaha ya kuficha na kufunikwa fedheha hiyo ya kushindwa Washington katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu amesema kuwa, kukataliwa muswada huo wa Marekani ni mafanikio ya kisiasa ya Iran na kufeli kisiasa na kisheria utawala wa Marekani. Amesema anatarajia kwamba, nchi za kanda hii zitapata somo na kujiweka mbali na utawala ghasibu na dhalimu wa Israel.
Rais Rouhani amelaani hatua ya Imarati ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema: Hatua hiyo ya Imarati ni kosa kubwa na usaliti kwa malengo ya Wapalestina na Quds tukufu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatahadharisha watawala wa Imarati wasiifungulie Israel mlango wa kuingia katika eneo hili na kusema: Watala wa UAE wanapaswa kuwa macho na kuzinduka kutokana na kosa kubwa na usaliti walioufanya, na wasiendeleze njia hiyo isiyo sahihi.
342/