Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ofisi ya Shirika la Afya Duniani imetangaza kuwa, kiwango cha maambukizi ya corona na ukali wake havijabadilika tangu miezi sita iliyopita.
Ofisi ya WHO imeongeza kuwa, haijui lini mgogoro wa corona utamalizika lakini inakadiriwa kwamba ugonjwa wa COVID-19 utadhibitiwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Taarifa ya Ofisi ya WHO imesisitiza kuwa, ukali wa magonjwa yanayosababishwa na virusi vinavyowapata wanadamu unaongezeka na kupungua lakini uchunguzi uliofanyika unaonesha kuwa, maambukizi na ukali wa COVID-19 haujabadilika.
Takwimu za mtandao wa worldometers.info zinaonesha kuwa watu 28,366,652 wameambukizwa virusi vya corona kote dunia na 914,501 miongoni mwao wameaga dunia kutokana na virusi hivyo.
Kwa sasa Marekani inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi vya corona na vilevile idadi kubwa zaidi ya watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo. Hadi sasa zaidi ya Wamarekani milioni sita na nusu wamepatwa na corona na wengine karibu laki mbili wameaga dunia kwa ugonjwa wa COVID-19.
342/