Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Tarehe 31 mwezi Shahrivar katika kalenda ya Iran inaashiria kuanza Wiki ya Kujitetea Kutakatifu hapa nchini. Jeshi vamizi la utawala wa Saddam Hussein, dikteta aliyeng'olewa madarakani huko Iraq, tarehe 31 mwezi Shahrivar mwaka 1359 Hijria Shamsia sawa na mwezi Septemba mwaka 1980, lilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Iran kwa kutumia aina mbalimbali za silaha likidhani kwamba katika muda wa wiki moja tu lingeweza kuudhibiti mji wa Tehran.
Rais Hassan Rouhani ametangaza leo katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Wiki ya Kujitetea Kutakatifu kuwa, kujitetea kutakatifu kunakumbusha irada thabiti, kuwa huru na kujitolea wananchi ambao waliweza kubakisha hai kumbukumbu ya ushindi wao mkubwa katika historia, na matokeo yake yameongeza ufahamu na muono wa mbali katika kukabiliana na maadui.
Rais Rouhani amesema kuwa, katika njia za jihadi na muqawama mashahidi walionyesha njia ya haki, kupenda uadilifu na uhuru; na kuuawa kwao shahidi na kujitolea mhanga kulizidisha na kueneza zaidi mafundisho na tahamni aali za Uislamu. Amesema, mashahidi ni kigezo cha daima kwa jamii zote za Kiislamu na wanadamu waopigania uhuru duniani.
342/