Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Bw. Hossein Amir Abdollahian aliandika hayo jana katika ukurasa wake wa Twitter na kuongeza kuwa, kuheshimu haki ya kujitawala kila nchi, kusimamishwa haraka vita na kufanyika mazungumzo ya kisiasa ndizo njia pekee za kukomesha mgogoro wa eneo hilo baina ya Jamhuri ya Azerbaijan na Armenia.
Amesisitiza kuwa, kulindwa kikamilifu usalama katika mipaka ya Iran ndicho kipaumbele kikuu cha Tehran na kwamba Iran haina mchezo hata kidogo katika suala hilo.
Nchi mbili za Jamhuri ya Azerbaijan na Armenia zina mogogoro baina yao kuhusu eneo la Karabakh. Mgogoro huo ambao unachochewa zaidi na uingilia wa nchi za kigeni, ulianza mwaka 1988 na mwaka 1991 kulitokea vita baina ya nchi hizo mbili.
Vita vinavyoendelea hivi sasa vilianza Jumapili iliyopita kwa mashambulizi makali baina ya majenshi ya pande mbili na hadi sasa watu kadhaa wameshauawa na kujeruhiwa.
Dk Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Jumapili usiku alizungumza kwa simu katika nyakati tofauti na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Armenia na Jamhuri ya Azerbaijan na kuzitaka nchi hizo kuvumiliana, kusimamisha haraka vita na kuanza mazungumzo kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
342/