7 Oktoba 2020 - 11:17
Taarifa ya mataifa 26 ya dunia ya kulaani vikwazo vya upande mmoja vya Marekani

Marekani ikiwa na lengo la kusukuma mbele gurudumu la siasa zake za kigeni inashikilia rekodi ya kuwa dola lililoyawekea mataifa mengine ya dunia vikwazo vya upande mmoja.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Vikwazo hivyo vimekuwa vikitekelezwa kwa kutumia visingizio mbalimbali hususan kupinga siasa na hatua za Washington. Sambamba na hayo, katika baadhi ya mambo kama vikwazo dhidi ya Russia, madola ya Magharibi nayo yamekuwa pamoja na Marekani. Jambo hilo limekabiliwa na upinzani mkali wa mataifa ya dunia.

Mataifa 26 ikiwemo Iran, Syria, Russia, China na Iraq yametoa taarifa ya pamoja na kutangaza kuwa, vikwazo vya kiuchumi vya upande mmoja na vya kidhalimu vya Marekani na baadhi ya madola ya Magharibi dhidi ya mataifa huru na yasiyokubali kuburuzwa, vimegeuka na kuwa kizingiti kikubwa katika kukabiliana na virusi vya Corona.

Taarifa ya pamoja ya mataifa hayo, ilitolewa Jumatatu ya juzi katika kikao cha tatu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichokuwa maalumu kwa ajili ya masuala ya haki za binadamu kilichoitishwa na mwakilishi wa China katika umoja huo.

Mataifa hayo yametoa wito wa kuhitimishwa vikwazo vya kiuchumi vya upande mmoja vya Marekani na baadhi ya madola ya Magharibi dhidi ya baadhi ya nchi na kusisitiza kwamba, hatua ya mataifa hayo ya kutekeleza vikwazo mbali na kuwa inakiuka haki za binadamu, ni kiziuzi kikubwa katika kukabiliana na virusi vya Corona.

Marekani ndilo taifa linaloongoza kwa kuyawekea vikwazo mataifa mengine ya dunia na imekuwa ikitekeleza mbinu hiyo ya vikwazo kwa ajili ya kufikia malengo yake ya kisiasa. Baadhi ya mataifa waitifaki wa Marekani nayo yamekuwa yakiungana na Marekani katika vikwazo hivyo.

Vikwazo hivyo vimekuwa vikitekelezwa kwa kutumia visingizio mbalimbali lakini kubwa zaidi ni kupingana na siasa za Washington. Marekani haitaki kabisa kuona inapingwa na kuambiwa hapana. Na ndio maana mataifa yasiyokubali kuipigia magoti Marekani na kuwa yenye kuitii siku zote yamekuwa yakishinikizwa na kuandamwa na vikwazo vya Washington.

Hata katika kipindi hiki nyeti na hatari cha kuenea virusi vyay Corona ulimwenguni, Marekani imeweka kando kabisa ubinadamu kutokana na kushadidisha vikwazo vyake.

Marekani mbali na kuiwekea vikwazo vikali zaidi Iran ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika historia katika fremu ya kile kinachojulikana kama siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa, imeziwekea vikwazo vingi na vya upande mmoja nchi kama Russia, China, Venezuela, Cuba, Syria na Korea Kaskazini.

Pamoja na hayo, vikwazo hivyo vya Marekani vinazidi kukabiliwa na malalamiko na upinzani mkubwa katika pembe mbalimbali za dunia. Hii leo hata ndani ya Marekani kwenyewe mbali na kushuhudiwa upinzani dhidi ya serikali ya Rais Donald Trump, kunatolewa miito ya kuondolewa vikwazo hivyo vya kidhalimu na visivyo vya kibinadamu dhidi ya mataifa mengine.

Kwa kuzingatia kuweko taathira hasi na haribifu kutokana na kuendelea vikwazo hivyo vya upande mmoja vya Marekani, inaonekana kuwa, ukosoaji na kuchukuliwa hatua za pamoja za mataifa ya dunia dhidi ya Washington kutokana na dola hilo kutekeleza hayo bila ya idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni jambo la dharura mno, ili kuifanya Marekani ilazimike kuangalia upya maamuzi yake hayo.

342/