Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa taarifa kundi moja la wanafunzi Wairani nchini Ufaransa liliwasilisha pendekezo la kuchapisha stempu iliyoandikwa "Nampenda Muhammad" kwa ajili ya kumuenzi Mtumu Mtukufu wa Uislamu, Muhammad SAW, lakini Idara ya Posta ya Ufaransa (La Poste) imekataa kata kata ombi hilo.
Idara ya Posta ya Ufaransa imedai kuwa stempu iliyoandikwa 'Nampenda Muhammad" ina mielekeo ya kidini na hivyo haikubaliki.
Kwa mujibu wa sheria za Ufaransa, kila mtu nchini humo anaweza kupendekeza stempu maalumu itakayotumika katika shughuli za posta. Hata hivyo La Poste imekataa kuchapisha stempu ya "Nampenda Muhammad."
Hayo yanajiri wakati ambao matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akidai kwamba Uislamu uko kwenye mgogoro duniani kote na msimamo wake wa kuunga makono kitendo kiovu cha jarida la nchi hiyo la Charlie Hebdo cha kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW yameughadhibisha Ulimwengu wa Kiislamu. Macron ametangaza kuwa Ufaransa itaendelea kuchapisha vibonzo hivyo huku akidai kuwa kuvunjiwa heshima Uislamu ni katika fremu ya uhuru wa kujieleza.
Maandamano makubwa yamefanyika na yanaendelea kufanyika katika nchi mbalimbali kulaani msimamo huo wa Macron. Mbali na maandamano, zinaendeshwa kampeni pia za kususia bidhaa za Ufaransa.
342/