Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: limenukuu duru za kuaminika zikisema kuwa, wanasaikolojia wa usalama wa Marekani kwa kushirikiana na vikosi vya kiintelijensia vya utawala haramu wa Israel wanasajili na kuwapa mafunzo ya kijeshi watu wa familia za wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) walioko katika kambi ya wakimbizi ya al-Hol katika mkoa wa al-Hasakah kaskazini mashariki mwa Syria.
Inaarifiwa kuwa, familia hizo mbali ya kupewa mahitaji ya msingi ya kila siku na Marekani, Uingereaza na Israel kambini hapo, lakini zinapewa pia vitabu vya kitakfiri kama kile kiitwacho 'Taifa la Ibrahim' kilichoandikwa na al-Maqdisi. Kitabu hicho cha 'The Nation of Ibrahim' kimetumika pia katika kambi ya Bucca katika mji wa Ummul Qasr katika mkoa wa Basra kusini mwa Iraq kuunda kizazi kipya cha ISIS (ISIL 2).
Habari zaidi zinasema kuwa, Marekani na Wazayuni wanafanya juu chini kuwarubini wanawake na vijana kujiunga na kizazi hicho kipya cha ISIS katika nchi za Iraq na Syria.
342/