Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Majid Takht Ravanchi alisema hayo jana Jumamosi na kuongeza kuwa, Trump amefanya mambo mengi ya kuishangaza dunia katika miaka kadhaa iliyopita, na kwamba Iran ya Kiislamu itaendelea kuwa macho hata katika siku hizi chache za utawala wake.
Amesema Jamhuri ya Kiislamu haina wasi wasi wowote kuhusu habari zinazoenea kwamba kuna uwezekano Trump akaamua kutumia silaha za nyuklia dhidi ya taifa hili ndani ya siku chache za uongozi wake.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran ameeleza bayana kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haitarajii makubwa kutoka utawala ujao wa Marekani, historia inaonesha kuwa, dola hilo la kibeberu liwe chini ya utawala wa Democrats au Republican, limekuwa na sera za nje zilizojaa uhasama dhidi ya Iran.
Amesema hakuna shaka kuwa utawala ujao wa Marekani wa Joe Biden utaendeleza sera za vikwazo dhidi ya Tehran lakini kwa mkondo na mbinu tofauti.
Wiki iliyopita, Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusiana na chokochoko za kijeshi zilizoanzishwa na Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi akisisitiza kwamba: Iran haitaki kuanzisha vita, lakini haitafanya ajizi katika kulinda watu wake, usalama na maslahi yake ya taifa.
342/