15 Machi 2021 - 10:41
Zakhrova: Magharibi haina uthubutu wa kuishambulia Russia kutokana na mifumo yake imara ya kiulinzi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameweka wazi kuhusu uwezo wa kiulinzi wa nchi hiyo na kusema: Magharibi hivi sasa inaendesha vita vya kiintelijinsia dhidi ya Russia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Maria Zakharova ameeleza kuwa, nchi za Magharibi hazina uthubutu wa kuishambulia moja kwa moja Russia kwa sababu katika miaka ya karibuni Russia imeunda mfumo wa kujilinda ambapo ni kazi ngumu kwa nchi hizo kutekeleza jambo hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Ijumaa iliyopita pia alitahadharisha juu ya hatua ya Marekani ya kuweka ngao yake ya makombora huko Japan. 

Aidha akizungumza na wanahabari katika kikao chake cha kila wiki, Bi Zakharova amesema: Iwapo Marekani itatuma makombora au kuweka ngao ya makombora huko Japan Russia nayo italipiza hatua hiyo ili kulinda usalama wake wa taifa. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametoa maelezo kuhusu suala hilo akisema: Kutumwa kivyovyote vile makombora ya masafa mafupi na ya kati katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo katika eneo la Asia-Pacific kuna athari kubwa katika kuyumbisha amani na uthabiti kwa upande wa usalama wa kimataifa na kieneo. Hatua hiyo itapelekea kuanza duru mpya ya mashindano ya silaha yenye taathira zisizoweza kutabirika. 


342/