Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Khalid Mash'al ameeleza kuwa, harakati ya Hamas itaendeleza juhudi kwa kustafidi na nyenzo na njia zote zinazowezekana ili kupunguza mateso na masaibu ya mateka wa Kipalestina na kuachiwa huru kutoka katika jela za utawala wa Kizayuni.
Ameongeza kuwa adui Mzayuni atalazimika kuwaachiwa huru mateka hao kwa lugha tu ya muqawama na si kupitia mazungumzo na majadiliano. Khalid Mash'al amesisitiza kuwa: sisi hatimaye tutamlazimisha adui Mzayuni kuwaachia wafungwa wa Kipalestina. Mash'al ameashiria namna jukumu kuu la Hamas na makundi mengine ya muqawama ya Palestina kuwa ni kuhakikisha kuwa mateka wanaachiwa huru kutoka katika jela za adui na kutaka kushadidishwa muqawama katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan kwa lengo la kukabiliana na uvamizi na jinai za adui Mzayuni. Amesema kuwa, ni kupitia muqawama pekee ndipo ardhi na mateka wa Kipalestina watakapokuwa huru.
342/