Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Netanyahu ametoa shukrani hizo sambamba na kutoa vitisho kwa mara nyingine tena dhidi ya makundi ya muqawama ya Palestina kwa kueleza kwamba, utawala wa Kizayuni utatoa pigo kali kwa makundi hayo.
Waziri Mkuu wa utawala katili wa Israel alitoa kauli hiyo Ijumaa jioni baada ya kikao alichofanya na wakuu wa mashirika ya usalama ya utawala huo wa Kizayuni na kuongeza kwamba jeshi la Kizayuni limezishambulia ngome za chini ya ardhi za makundi ya muqawama ya Palestina na kwamba mashambulio hayo yataendelezwa.
Netanyahu ametoa vitisho hivyo katika hali ambayo, Abu Hamza, msemaji wa brigedi za Sarayal-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amejibu vitisho vya utawala wa Kizayuni vya kuanzisha operesheni ya mashambulio ya nchi kavu dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa kusisitiza kuwa, mapambano ya nchi kavu ni njia ya mkato zaidi kwa muqawama kufikia ushindi na kwamba katika mapigano hayo, hatima ya wanajeshi wa Kizayuni itakuwa ni ima kutekwa au kuuawa.../
342/