Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mawaziri watatu wa Wizara ya Ulinzi, Sheria na Mashauri ya Kigeni walipata kura nyingi za Wabunge ikilinganishwa na mawaziri waliopendekezwa kushika wizara nyingine.
Amir Hussein Abdulahian, anachukua nafasi muhimu ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni huku Muhammad Ashtiyani akikabidhiwa Wizara ya Ulinzi.
Hossein Baghgoli, aliyependekezwa na Rais Raeisi kwa ajili ya kuchukua Wizara ya Elimu na Malezi hakuweza kupata kura za kutosha za Wabunge za kumuwezesha kuchukua usukani wa Wizara hiyo. Kwa muktadha huo, ni waziri mmoja tu kati ya mawaziri 19 ambao majina yao yaliwasilishwa Bunge ni kwa ajili ya kupigiwa kura ya kuwa na imani nao ndiye ambaye hakupasishwa. Sasa Rais Ibrahim Raesi analazimika kupendekeza jina jingine kwa ajili ya wizara hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupasishwa mawaziri hao, Rais Ibrahim Raeis amelipongeza Bunge kwa kupasisha mawaziri wake kwa wingi mkubwa wa kura na kueleza kwamba, hatua hiyo ni mwanzo mzuri wa ushirikiano wa Serikali na Bunge kwa ajili ya kuijenga Iran yenye nguvu.
Aidha akizungumza leo katika kikao chake cha kwanza na baraza lake la mawaziri, Sayyid Ibrahim Raeisi amesema, wananchi wa Iran wanapaswa kuhisi ustawi na maendeleo pamoja na utekelezwaji wa uadilifu. Amesema kuwa, katika baadhi ya sekta kuna hali ya kubakia nyuma kukubwa ambako kunapaswa kufidiwa.
342/