Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hayo yamedokezwa na Mohammad Hossein Fallah Mehrabadi, mkuu wa utafiti na teknolojia katika Taasisi ya Utafiti wa Chanjo ya Razi ambayo inatengeneza chanjo hiyo, ambaye pia ni msemaji wa mradi huo. Akizungumza Jumapili, amesema awamu ya tatu ya majaribio kwa wanadamu itafanyika katika mikoa ya Tehran na Alborz na kuwajumuisha watu 40,000 waliojitolea.
Fallah Mehrabadi amesema Taasisi ya Utafiti wa Chanjo ya Razi ilizalisha chanjo 400,000 mwezi uliopita na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa makadirio wataweza kuzalisha chanjo milioni 15 hadi million 20 za chanjo ya Razi Cov Pars hadi kufikia mwezi Machi mwakani.
Chanjo hii ni ya aina yake kwani ina dozi tatu. Dozi za kwanza mbili ni za kudungwa na dozi ya tatu ni tone linaloingizwa mwilini kupitia pua.
Tayari Iran imeshaanza kuzalisha chanjo yake ya kwanza ya COVIran Barekat ambayo sasa inatumika kwa wingi kote Iran huku ikisubiri idhini ya Shirika la Afya Duniani ili kuuzwa katika soko la kimataifa.
Iran iko mbioni kuunda chanjo kadhaa za COVID-19, ambapo mbali na chanjo hiyo ya COVIran Barekat na Razi Cov Pars chanjo zingine ambazo zimepiga hatua nzuri katika majaribio ni pamoja na Fakhra, Noora na chanjo ya pamoja ya Taasisi ya Chanjo ya Finlay ya Cuba na Taasisi ya Chanjo ya Pasteur ya Iran.
342/