Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika hilo linasema misako na kamatakamata inayofanywa na mamlaka mwezi huu inalenga maeneo yenye wakazi wengi wakimbizi na waomba hifadhi ambayo imesababisha vifo kadhaa, maelfu kuzuiliwa, na wengi wakiachwa masikini na bila makazi.
Vincent Cochetel, mwakilishi maalum wa UNHCR kuhusu hali ya eneo la Mediterranea ya Kati na Magharibi amesema tangu kuanza kwa misako na kukamatwa na maafisa wa Libya mwezi Oktoba, kumeshuhudia kuzorota kwa kasi hali inayowakabili wanaotafuta hifadhi na wakimbizi walio hatarini huko Tripoli. Ameitaka serikali ya Libya ije na mpango mzuri unaoheshimu haki zao na kubainisha suluhisho la kudumu.
UNHCR pia imetoa wito kwa mamlaka kuheshimu haki za binadamu na utu wa watu wanaoomba hifadhi na wakimbizi, waache kuwakamata kiholela na kuwaachilia wanaowashikilia kutoka kizuizini.
Kukosekana serikali kuu yenye nguvu huko Libya kumetoa mwanya wa kufanyika magendo mbalimbali yakiwemo ya binadamu na sasa hivi Libya ni njia kuu ya wahajiri haramu wanaoelekea barani Ulaya kwa tamaa ya kupata maisha bora. Uvamizi huo wa NATO umefungua njia pia ya kuingia Libya magenge ya kigaidi hasa Daesh (ISIS).
Libya imekumbwa na ukosefu wa usalama na amani tangu mwaka 2011 wakati jeshi la nchi za Magharibi NATO lilipofanya mashambulizi makali nchini humo wakati wa kampeni za kumng'oa madarakani kiongozi wa wakati huo Muammar Gaddafi.
342/