Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: WHO imeeleza katika ripoti yake mpya kwamba, ndani ya muda wa saa 36 hadi 72 maambukizi ya omicron huongezeka maradufu, jambo linaloonyesha kuwa spishi hiyo mpya inaongezeka kwa kasi zaidi kulinganisha na ile ya delta iliyokuwa imeenea zaidi hadi sasa.
Kutokana na hali hiyo, muda mfupi ujao spishi ya omicron itaizidi delta na kuwa kirusi kilichoene zaidi duniani.
Shirika la Afya Duniani limeongeza kuwa, idadi ya watu wanaolazwa hospitalini katika nchi za Uingereza na Afrika Kusini inaendelea kuongezeka; na kuna uwezekano, baada ya muda si mrefu, ongezeko hilo la kasi, la watu wanaoambukizwa kirusi cha omicron likasababisha mashinikizo makubwa kwa mifumo ya utoaji huduma za tiba.
Wakati huohuo Ujerumani imetangaza kuwa imeiweka Uingereza kwenye orodha ya nchi zenye mazingira hatarishi zaidi ya maambukizi ya Covid-19 na hivyo kuwawekea masharti magumu wasafiri wanaotoka nchini humo.
Uamuzi huo umechukuliwa huku omicron kikitangazwa kuwa ndicho kirusi kilichosambaa kwa wingi zaidi katika mji mkuu wa Uingereza, London, ambapo asilimia 60 ya watu waliogundulika kuwa na virusi vya corona nchini humo wamekutwa na spishi hiyo mpya ya kirusi cha corona.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ametahadharisha kuwa hadi ifikapo katikati ya mwezi Januari mwakani, kirusi cha omicron kitakuwa ndicho kilichosambaa zaidi katika nchi za bara hilo.../
342/