Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa duru hizo, miripuko mitatu imetokea mapema leo huko Tel Aviv na bandari ya Yafa.
Kuhusiana na matukio hayo, jeshi la utawala wa Kizayuni nalo pia limetangaza kuwa limepokea ripoti kuhusu kufyatuliwa makombora kutoka Ukanda wa Gaza na kwamba linaendelea kuchunguza suala hilo.
Halikadhalika, Polisi ya utawala haramu wa Kizayuni imesema imepokea ripoti za kutokea mripuko karibu na pwani ya Tel Aviv.
Baadhi ya duru za Palestina zimetangaza kuhusiana na suala hilo kuwa, inavyoonekana, milio hiyo ya miripuko iliyosikika ni ujumbe na indhari ya makundi ya Palestina katika Ukanda wa Gaza kuhusu mateka Mpalestina Hisham Abu Hawash anayeshikiliwa katika jela ya utawala wa Kizayuni, ambaye hali yake ni mahututi baada ya kususia kula kwa muda wa siku 138 sasa.
Hadi tunaingia mitamboni hakukuwa na taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu miripuko hiyo.../
342/