Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Lavrov ameyasema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian yaliyofanyika jana mjini Moscow.
Amir-Abdollahian ameandamana na Rais Ebrahim Raisi ambaye ameongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika safari ya kuitembelea Russia kwa mwaliko wa Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameeleza kwamba, marais wa nchi mbili walikuwa na mazungumzo marefu na ya kina na akaongeza kuwa, ratiba ya safari ya Rais wa Iran imejumuisha mambo mengi ikiwemo hotuba yake katika bunge la nchi hiyo Duma.
Marais Ebrahim Rais wa Iran na Vladimir Putin wa Russia walikutana na kufanya mazungumzo mjini Moscow siku ya Jumatano.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyaelezea mazungumzo ya marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa Twitter akisema: "katika kikao muhimu kilichofanyika Kremlin katika anga ya urafiki na kuchukua muda mrefu baina ya Raisi na Putin, uhusiano wa Tehran na Moscow umechukua mkondo mpya, wa kasi kubwa na wa masuala mbalimbali".../
342/